Jumatano, 5 Septemba 2018


UMUHIMU WA ASALI NA SIFA ZA ASALI MBICHI.
Tambua ya kuwa asali inavirutubisho maradufu katika afya zetu sisi Wanadamu, ni asali ambayo inatibu mengi kutokana na virutubisho vyake mwilini mwetu.

1. Ukitumia asali mara kwa mara, mwili wako utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye asali.

2. Ukilamba asali, utajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili wako kwa ujumla.

3. Ulaji wa asali huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo(Constipation), au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia.

4. Ukilamba asali, mwili utapata nguvu na kukuondolea uchovu ndani ya nusu saa tu, kwa sababu asali ina sukari ya asilia kama.

N.B.Ili kupata faida zaidi za asali, changanya na maziwa fresh kisha tumia kama kinywaji. Unapojisikia mchovu badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu ramba asali, hata kiasi cha vijiko vitatu tu vinatosha.

5. Asali ina madini pia aina ya potassium¡ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji kiasi wa potassium huweza kumuepusha mtu na kupatwa na kiharusi (stroke).

6. Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia), wanaweza kupata ahueni kwa kula Asali/ tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu vitamu vingine huozesha meno, utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.

7. Kwa tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, changanya asali na mdalasini kisha lamba asubuhi kabla haujala kitu chochote na mchana kabla ya kula na usiku kabla ya kula pia na kabla ya kulala

8. Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha. Asubuhi, zisage tende hizo kwenye maziwa hayo hadi zichangayike, kisha weka asali kiasi cha vijiko vitatu au vinne vikubwa pamoja na unga wa hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo. Kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.

9. Asali ni dawa ya unene, kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende asali kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina maana kwamba, wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa. Pia Asali husaidia uondoaji wa kilevi mwilini.

10. Asali inatibu saratani ya tumbo. Habari njema kuhusu Asali kama tiba ni kwamba, haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa asilia na inafanyakazi vizuri kuliko dawa
za kisasa¡. Asali vile vile ina imarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).

HAKIKISHA ASALI IWE MBICHI NA HAJACHANGANYWA NA MAJI AU KITU CHOCHOTE.
Kuna njia nyingi za kupima asali kuwa ni mbichi au imechanganywa na maji au vitu vingine.Nimechagua njia kuu mbili, leo tutaanza na moja kisha baadae tutamalizia njia nyingine.
Vipimo ili ujue asali ni mbichi;-
1.  Asali inatabia ya kuwaka, kwa sababu hiyo tunatumia njia ya kuwasaha moto kwa njiti ya kiberiti na njiti ya kiberiti kuiwasha asali ili iwake kama haijachanganywa na kitu chochote au maji..n.k.
MAHITAJI.
1. Njiti ya Kiberiti
2. Kiberiti
3. Asali.

NAMNA YA KUFANYA JARIBIO.
Chukua njiti ya kiberiti, loweka upande wa baruti ya njiti hiyo kwenye asali kisha washa kwenye kibiriti.

 MATOKEO

1.Njiti ikiwaka kwa kutatarika basi ni ishara kwamba asali hiyo inawaka kwa maana ya kwamba ni mbichi na ndiyo inayofaa kwa afya ya matumizi ya Mwanadamu.

2. Njiti isipowaka maana yake ni kwamba asali inamaji au imechemshwa, iliyochemsha maana yake ni kwamba joto limevunja muunganiko wa elementi za asali (Honey bond) kwahiyo asali iliyochemshwa haina tofauti na asali iliyochanganywa na maji, asali iliyo na vitu hivyo sio nzuri kwa matumiz ya Binadamu.



KARIBUNI KWA ASALI MBICHI YENYE UBORA
NAPUR HONEY-NATURAL AND PURE FRESH HONEY
Bei ni nzuri kabisa.
0717630811/0765611358
Email.bonaventuremashimbi@ gmail.com
UBORA WA KITU HUENDA SAMBAMBA NA ELIMU KWA WATU KUHUSU UBORA HUO.
ELIMISHA WENZAKO KUHUSU UBORA WA ASALI KAMA NILIVOFANYA.
WATUMIE WENZAKO WAJUE UMUHIMU WA ASALI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni