ASALI inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia
kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo
yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa
lishe na vifaa tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa asali kutibu unaweza
kuongezekan maradufu kama itachanganywa na mdalasini.
Aidha, uchunguzi wa kila wiki unaofanywa na jarida la World News kuhusu
tiba unasema, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea,imeonekana kwamba
kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini katika kujenga afya
bora.
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya
mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika
katika dawa ya Dork.
Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa
dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed
na Eric Vogelmann, madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini
yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya
chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.
Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri
linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994.
Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwamba matumizi ya kila siku ya asali
yanapunguza viwango vya lehemu mwilini.
Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika,
ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni kiungo muhimu katika
utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya
vipodozi na mafuta ya kupaka.
Ugonjwa wa mafua ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha
imegundulika na wataalamu kwamba hupungua na kupotea kabisa ikiwa
watatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na
robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mtafiti mmoja wa Hispania
imethibitisha kwamba, aina ya dawa moja asilia iliyofanikiwa kuharibu
vimelea viletavyo mafua ilitengenezwa kwa kiwango kikubwa na asali.
Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa
chafya na kuvimba kwa koo. Asali inaaminika pia huamsha hamu ya tendo la
ndoa. Wale ambao mambo katika eneo hilo si mazuri wanashauriwa angalau
kunywa vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku.
Kuna wakati asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini
za Mashariki mwa dunia ili isiwe sababu ya kuwaongezea mihemko.
Asali inaaminika kuwa dawa ifaayo katika kuondoa mchafuko wa tumbo
pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza
kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji, itapunguza
hali hiyo na maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
Utamaduni wa kula asali pamoja na mdalasini, huweza kuondoa mchafuko wa
tumbo na utumbo uletwao na gesi kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi
uliofanywa huko India na Japani kwa miaka mingi. Unaweza kukinga kupata
ugonjwa wa moyo na kuzuia, mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye
mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara wakati wa
kifungua kinywa.
Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku nyuzi
nyuzi zake ni muhimu pia kiafya. Tiba hii, iliweza kupunguza kuganda kwa
mishipa ya damu kwa asilimia 74 ya wagonjwa waliofanyiwa utafiti.
Shinikizo la damu, pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua
na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu
baada ya watafiti wa Kiitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali
iliyochanganywa na mdalasini.
Kinga ya mwili, itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara
asali na mdalasini kwa pamoja, wataalamu wanasema. Utafiti wa kitiba
unaonesha kwamba, asali ina hazina kubwa ya virutubisho na madini pamoja
na michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga, itolewayo
na chembechembe nyeupe za damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na
kuharibu vimelea virusi na bakteria. Vijiko viwili vya asali
iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo, huondoa kiungulia pia.
Inasemekana kuwa, unaweza kuishi hadi miaka 100 ukifurahia maisha ya
afya bora na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai
iliyowekwa mdalasini na asali.
Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vinne vikubwa vya
mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10, kunywa
robo kikombe kutwa mara tatu au nne, watafiti wanasema.
Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu wenye shida ya chunusi. Ili
kutibu tatizo hilo watafiti wanasema changanya vijiko vitatu vya asali
pamoja na kijiko kimoja mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika
muda wa wiki mbili pekee. Asali, wanasema inairudisha ngozi
iliyoharibiwa na wadudu waharibifu kama dondola, washawasha na hata
ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na
mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati
mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.
Utafiti uliofanywa karibuni nchini Australia na Japan, umeonesha kuwa,
asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa kwa mtu anayetumia madawa
ya kutibu saratani.
Katika utafiti uliofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango
kikubwa saratani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku
dozi za asali na mdalasini, walionesha kupata nafuu maradufu kuliko wale
waliokuwa wakitumia madawa ya saratani pekee.
“Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi,”
anasema Dk Hiroki Owatta. Upo ushahidi mpya kwamba, sukari asilia
zilizopo kwenye asali, zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini.
Zikitumika ipasavyo, sukari hizi