NJIA
ZA KUTAMBUA ASALI MBICHI.
SEHEMU
YA PILI.
NJIA
YA KUTUMIA KARATASI.
Utangulizi.
Njia hii hutumika kutambua asali
mbichi,njia hii inatumika kutokana na sifa za asali mbichi hivyo tunapima sifa
za asali mbichi kama ipo kwenye asali inayopimwa na ikionekana kuwa sifa hiyo ipo basi asali hiyo ni mbichi na ikionekana sifa hiyo haipo basi asali hiyo sio
mbichi.
SIFA
HUSIKA.
1 Asali
inamuunganiko wa kikemikari(Bond) ulio imara sana kiasi kwamba hautoi
kimiminika nje, elementi zake zimeshikamana kwa uimara sana hadi kutokutoa
kimiminika nje ya muunganiko huo.
Muunganiko
huo ni sifa asili ya asali kwahiyo asali yoyote iliyo mbichi inasifa hiyo,
muunganiko huo unaweza kuvunjwa kwa KUCHEMSHA ASALI, KUCHANGANYA ASALI NA MAJI.
Kwa
kuchemsha asali, elementi ndogondogo za asali zilizokua zimeshikamana huvunjika na
zikivunjika ndipo muungano ule unaporuhusu kimiminika kutoka nje ya muungano
hatimaye asali husika kuwa na maji, asali ikichemshwa uasilia wake unaharibika
hatimaye ubora stahiki unatoweka.
Kwa
kuchanganya na maji, muunganiko wa elementi za asali unavunjika kwa kutokea nje
na hatimaye ubora wa asali kuharibika kwa sababu hapo kunakua na mchanganyiko
wa asali na maji wa moja kwa moja.
MAHITAJI.
1 Karatasi
nyeupe.( Hakikisha karatasi hiyo ni Kavu)
2 Asali
itakayopimwa.
Namna ya kufanya jaribio hilo -;
- Chukua karatasi yako safi ambayo ni kavu(Hakikisha karatasi hiyo ni kavu) na uiweke sehemu ambayo ni flat kama mezani.
- Chukua asali kisha mimina tone la asali juu ya karatasi hiyo.
- Acha kwa muda wa dakika 45 mpaka saa moja.
Kimsingi
karatasi ikiwekewa maji huloana, sasa kwakua asali inamuunganiko wa elementi
zake ulio imara na ambao haupitishi kimiminika yaani umeshikamana(Compact) basi asali
itakapomiminwa kwenye karatasi hata ikikaa muda mrefu kiasi gani kama asali
husika ni mbichi basi karatasi hiyo haiwezi kuloana upande wa pili lakini kama
asali hiyo ina kimiminika kama maji basi karatasi hiyo italoana upande wa pili.
Tuendelee kufwatilia
mwendelezo huu, toleo linalofuata tutaona njia ya tatu, ambayo ni njia ya maji....
KARIBUNI KWA ASALI MBICHI YENYE UBORA
NAPUR HONEY-NATURAL AND PURE FRESH HONEY
Bei ni nzuri kabisa.
0717630811/0765611358
Email.bonaventuremashimbi@gmail.com
UBORA WA
KITU HUENDA SAMBAMBA NA ELIMU KWA WATU KUHUSU UBORA HUO.
ELIMISHA
WENZAKO KUHUSU UBORA WA ASALI KAMA NILIVOFANYA.
WATUMIE
WENZAKO WAJUE UMUHIMU WA ASALI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni